Ads 468x60px

SOCIAL FLOATING

Get this

Saturday 23 August 2014

Sunday 6 January 2013

KESHO NI UJIO WA NGOMA MPYA YA ROMA MKATOLIKI IITWAYO "2030"

Baada ya kukaa kimya kwa zaidi ya mwaka bila kutoa ngoma mpya, hatimaye rapper Roma anatarajia kutoa ngoma yake mpya kesho Ijumaa. Ngoma hiyo inaitwa 2030 na kama kawaida yake amezungumza masuala mengi pamoja na kutaja majina ya watu wengi maarufu kwa kuoanisha na matukio. Hit ya mwisho aliyoitoa Roma ni Mathematics.

HUU NDO UHASAMA NA CHUKI BINAFSI ZA WASANII WETU

TID vs Ali Kiba Beef hii ilianza baada ya Ali Kiba na familia yake kumshutumu TID kuwa alikuwa amepanga njama za kumuua Ali Kiba. Tuhuma hizo zilipelekea TID kupelekwa polisi lakini alitoka baada ya kesi hiyo kuonekana haina ushahidi wa kutosha. Mpaka sasa TID bado ana hasira na Ali Kiba na hivi karibuni kupitia Facebook alimuita ‘homo’ kutokana na kitendo chake cha kumtupia shutuma hizo. “Stupid Thing Ever Happened in Bongo Music Scene is this Homo mentioned me Trying to Kill Him while am only thinkin about this Girl…No Homo,let’s make Hits,” aliandika TID. AY vs Hermy B
Uhusiano kati ya Hermy B na AY waliokuwa maswahiba wa muda mrefu uliingia dosari baada ya kile kinachodaiwa kushindwa kuelewana katika bei mpya ya kurekodia wimbo katika studio za B’Hits. Hermy B aliwataka AY na MwanaFA kulipia kiwango kikubwa zaidi kwa single wanazorekodi kwakuwa wao ni wasanii wakubwa kitu ambacho hawakukikubali na kuamua kuvunja uhusiano na B’Hits. Baadaye Hermy B alikuja kuandika barua mbili tofauti kuelezea jambo hilo na jinsi uhusiano wao ulivyovunjika. AY alidai angekuja kuandika maelezo kwa upande wake lakini hata hivyo hakuandika. Miongoni mwa aliyoandika Hermy kwenye barua ya kwanza ni: Kilichotokea ni kwamba, mwaka huu mwanzoni kabisa, A.Y aliwasiliana na mimi akiwa na mipango ya kuzindua albamu yake. Na alitaka kuzinunua zile nyimbo kutoka kwangu akiwa na mpango mpya wa kuiuza albamu kwa mpango wake binafsi pasi na mimi. Nilishindwa kuelewa nini anakifanya hasa alipoomba alipie wimbo mmoja mmoja tena kwa bei ya msanii wa kawaida anaehangaika kutoka. Niliamua kukubali kwamba ameamua kufanya hivyo na sina nguvu ya kumzuia basi nikajaribu kupata malipo halisi ya kazi yangu. Ubishi wangu ulikua kwamba msanii mdogo hawezi kulipa bei sawa ya kurekodi na msanii mkubwa, kwani hata malipo ya msanii mkubwa na mdogo baada ya kazi yoyote iwe ya matangazo ama show huwa hayafanani. Bei niliyotaja haikua millioni kumi, ni uongo mtupu na kwa wimbo mmoja niliomba nilipwe millioni 2. Akakubali kwa bei hiyo ya Millioni 2 japo nilihisi hakuridhika kabisa. Nilimtumia mkataba wa makubaliano yetu ambayo kweli baadae aliona kwamba bei hiyo kwake ni kubwa sana hivyo hatukusaini makubaliano. Tulibadilishana meseji kwa simu kwa muda mrefu sana na niliona biashara hii itavunja urafiki wetu. Nilifikiria sana kwamba nyimbo hizi nimekaa nazo toka 2008 bila kuingiza chochote na maisha yanaenda pia. Sikuona sababu ya kuharibu urafiki wetu wa muda mrefu kwa mabishano haya. Kwa Ujumbe wa simu nilimueleza A.Y anakaribishwa aje achukue nyimbo zoooooote anazohitaji kwa albamu yake BURE (bila malipo).Lakini nilimuomba anisamehe sitomix zile ambazo bado hazijamixiwa, ila ampatie producer mwingine amfanyie hiyo kazi. Mpaka naona hii makala A.Y hajaja kuchukua hizo nyimbo na ndio naelewa kua hayupo na BHits tena na wala taarifa zote hizo mbili hajawahi kunipatia. Huu ndio ukweli halisi. Lord Eyez vs Ommy Dimpoz
Beef hii ilianza baada ya Ommy Dimpoz kupost picha za Lord Eyez kwenye mtandao wa Twitter akiwa amekamatwa kwa kile alichodai kumuibia vifaa vya gari yake. Picha hizo zilisambaa kwa kasi kwenye mitandao ya kijamii na websites/blogs. Baadhi ya watu walimlaumu Ommy kwa kitendo hicho cha kumwanika mwanamuziki mwenzie. Baada ya kukamatwa na polisi na baadaye kutoka nje kwa dhamana wakati kesi hiyo ikiendelea, Lord Eyez alirekodi wimbo Bongo Records ambamo anasikika akimtaja Ommy Dimpoz.

P-SQUARE WAAPA KUTOKANYAGA TENA ARDHI YA UGANDA

Licha ya kupiga show ya nguvu mjini Kampala, Uganda mwezi uliopita, wasanii wa kundi la P-Square wamedaiwa kuapa kutokanyaga tena ardhi ya Uganda kwaajili ya show. Uamuzi huo wameuchukua baada ya kudaiwa kushikiliwa kwa masaa kwenye hoteli ya nyota 5 waliyokuwa wamefikia kwa kushindwa kulipa bili. Waandaji wa show hiyo walikataa kulipa bili hiyo kutokana na kuwa kubwa mno.Kwa mujibu wa vyanzo, mapacha hao Peter na Paul walisaini mkataba na mapromota hao na walilipwa gharama ya kufanyia show huku zile za malazi na usafiri zikiachwa. Hata hivyo kulikuwa na kiwango cha mwisho ambacho wasanii hao walitakiwa kukitumia pale walipofikia lakini walizidisha na hivyo waandaji kuwataka walipe wenyewe na hivyo kuleta mgogoro mkubwa. Wasanii hao wa Alingo walichukizwa na kitendo hicho na sasa wameahidi kutoenda nchini Uganda tena!!

PROFESA JAY ADAIWA KUMTAPELI PROMOTA WA MOMBASA KENYA

Kwa mujibu wa gazeti la The Star ka nchini Kenya, rapper Joseph Haule aka r Profesa Jay hivi karibuni aliingia kwenye mgogoro na promoter wa mjini Mombasa Kenya aliyemchukua kufanya show. Prof alikuwa amechukuliwa kufanya show mbili siku ya Christmas kwenye kumbi za Jamboree Resort na Quetu Beach Resort. Inavyodaiwa Profesa Jay hakuwa amelipwa fedha zote kwa show ya pili na hivyo alipewa camera aina ya Nikon D3000 kama rehani.Baada ya show, Prof aliondoka nchini Kenya na crew yake na kuibeba kamera hiyo. Sasa waandaaji hao wanadai kuwa walimpatia Prof hela yake iliyokuwa imesalia. Issue hiyo imekuwa kubwa kiasi ambacho passport ya mpambe aliyekuwa amesafiri na Jay nchini humo imeshikiliwa ili asiondoke.Waandaaji wanadai kuwa walimlipa Profesa Jay shilingi 252,000 za Kenya ambazo ni zaidi hata ya fedha walizokuwa wamekubaliana na sasa wanataka warudishiwe fedha yao. Polisi wanashughulikia kesi hiyo na Prof aliyekuwa ameingia makubaliano ya show nyingine katika ukumbi wa Jamboree December 31 aliitosa show hiyo.

PRODUCER LUCCI AKERWA NA DHARAU ZA WATANGAZAJI WA BONGO

Kupitia Twitter producer wa Tanzania aliyewahi kutengeneza beats za hits kadhaa ukiwemo Problem wa Cpwaa, Lucci amesimulia kiasi cha mtangazaji wa radio aliyejifanya kumsahau jina wakati wanafahamiana na alishamfanyia interview. Hata hivyo hajamtaja ni nani wala kitu cha radio anachofanyia kazi. Lucci ameandika: Aiseee jana kuna jambo limenikuta sasa sijui kama ilikua huyu radio presenter alikua HIGH KINYAMA au ni DHARAU KUPITILIZA…mtanisaidia. Nilikua naingia supermarket jamaa akanipigia honi kama nikageuka akanipungia. I waved back. Wakati nnatoka nikamkuta nje tukaongea kidogo. Baada ya story kadhaa na ma “long time man..upo?”..akaniomba number ili aje studio coz naye anaishi mbezi..nikampa number na kuanza kusepa. Presenter huyu ambaye ashaa wahi kunifanyia interviews, na bata tukala wote na biti kuniomba,akatia “man..plz kama nikumbushe jina lako ivi” Ilikua ni dharaaauuuuuu, ni kweli jina kanisahauuuuuuu, au dude was just ridiculously high on another level?!?!?

JAY JAY OKOCHA kufilisika

Taarifa kutoka kwenye magazeti manne makubwa ya Nigeria zimeripoti kwamba mchezaji maarufu na wa siku nyingi nchini humo Jay Jay Okocha anazidi kufilisika kila siku na sasa anafanya muendelezo wa kuuza mali zake ambazo zilikua kitega uchumi kikubwa kwake. Captain huyu wa zamani wa timu ya taifa ya Nigeria ambae pia alizichezea Bolton Wanderers and Hull City tayari mpaka sasa ameshaiuza club yake maarufu Nigeria iitwayo Club 10 ambayo ameiuza kwa Producer Don Jazzy ambae ni producer aliewatoa wengi akiwemo D’Banj, na sasa anafanya kazi na staa Tiwa Savage.
Club 10 ni kiwanja maarufu sana kwenye mji wa Lagos ambapo kimehudhuriwa na mastaa kibao akiwemo Akon. Baada ya kuiuza hiyo Club, sasa hivi anauza nyumba yake nyingine iko Akute, Ogun State ambapo mpaka sasa imeripotiwa kwamba midfield Maestro yuko tayari kufanya mazungumzo ya kuanzia N17 million.
 
Powered By Blogger

Sample Text

life is all about showing people what you gat

Translate